The House of Favourite Newspapers

Diwani Mwingine CHADEMA Atimkia CCM

Diwani wa Kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru kwa tiketi ya Chadema, Wilson Nanyaro ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Nanyaro amekuwa diwani wa 11 katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kipindi hiki na kuhamia CCM ili kumuunga mkono Rais Magufuli.

 

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Emanuel Mkongo amethibitisha kupata taarifa za kujiuzulu udiwani kwa Nanyaro.

PIGO JINGINE CHADEMA, MBUNGE SERENGETI ATIMKIA KWA MAGUFULI – VIDEO

Comments are closed.