Dk. Fadhili adaiwa kumuingiza Wolper Freemason

DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELIDaktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dk. Fadhili Emily.

Mwandishi wetu

DAKTARI wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dk. Fadhili Emily amedaiwa kuwa ndiye mshirika mkubwa aliyemshawishi mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper kujiunga na taasisi ya siri ya Freemason.

wolper
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper

Miezi kadhaa iliyopita, mwigizaji huyo aliwahi kunaswa katika jengo la Freemason lililopo Posta jijini Dar ambapo alipoulizwa kuwa anaabudu katika jengo hilo, alikataa na kudai kulikuwa na mtu anamtafuta katika moja ya jengo lililo karibu na jengo hilo.

Kwa mujibu wa chanzo, Dk. Fadhili ambaye utajiri wake umekuwa ukitiliwa shaka na wengi kutokana na kumiliki magari na nyumba kadhaa za kifahari, ndiye aliyemshawishi kujiunga na taasisi hiyo na sasa wanaendelea kuabudu pamoja.

“Nyie kwani hamumjui Dk. Fadhili ambaye anadhamini mashindano yenu? Huyo ndiye anayedaiwa kumuunganisha Wolper Freemason.,” kilisema chanzo hicho.

Mara baada ya kupata taarifa hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Wolper kwa njia ya simu, hakupatikana lakini bahati nzuri Dk. Fadhili alipatikana na kutoa ufafanuzi wake.

“Mimi si Freemason na sijamuunganisha Wolper. Wolper tunafahamiana tu kama ninavyofahamiana na watu wengine. Katika taasisi yetu ya Fadhaget Sanitarium Clinic, tunawaajiri watu na kweli wanapata fedha, nyumba na magari lakini havihusiani na Freemason,” alisema Dk. Fadhili.


Loading...

Toa comment