The House of Favourite Newspapers

Dk. Mwinyi: Nivumilieni, Ninafanya Uamuzi Mgumu – Video

0

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, amewataka wananchi kumvumilia wakati akifanya uamuzi mgumu dhidi ya watu wanaoshiriki rushwa, uhujumu uchumi, ufisadi wa kutafuna mali za umma. Amesema hatovumilia watendaji wanaoshiriki vitendo vya rushwa vinavyoisababishia Serikali hasara.

 

Ameeleza hayo jana Alhamisi, Desemba 17, 2020 katika ukumbi wa Fidel-Castro Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wakati akitoa shukrani kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake pamoja na wazee na mabalozi wa chama hicho.

 

Amebainisha kuwa yapo mambo yasipofanywa kwa uamuzi mgumu huko mbele kutakuwa kugumu na yale maendeleo ambayo yamekusudiwa kufanyika hayatofikiwa.

 

Amesema katika maendeleo ya watu hatokuwa na utani kwani Zanzibar kila anayeguswa itaelezwa kuwa ni mtoto wa fulani ama ana undugu na watu fulani, “huku nchi ikiendelea kufilisiwa kwa vitendo vya uhujumu wa mali za umma.”

 

Amesisitiza kwamba  amekaa madarakani kwa mwezi mmoja na nusu lakini kila anapogusa kumejaa vitendo vya ufisadi. ”Nitafanya maamuzi magumu lakini sitofukua makaburi wala kutafuta mchawi, baada ya maamuzi hayo kila senti ya fedha za umma itaheshimiwa,.

 

Leave A Reply