The House of Favourite Newspapers

Queen Darleen Aukimbia Mjengo Wa Kifahari

0

HATA kama Waswahili wanaamini mwenda kwao siyo mtoro lakini kwa msanii wa Bongo Fleva na memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, vijembe vinamwandama baada ya kuonekana hivi karibuni akiishi kwao maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

 

Kurejea kwao kwa msanii huyo imekuwa habari ya mjini na kwenye mitandao ya kijamii hasa baada ya kuikimbia nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi na mumewe iliyopo ushuani Mbezi Beach, Dar na hivyo kuonekana kama amefulia.

 

Chanzo chetu kutoka ndani ya familia kinasema kuwa ‘Queen Darleen, ameondoka kwenye mjengo huo wa maana kwa sababu anadaiwa kodi ya miezi sita, jambo lililomfanya mwenye nyumba kumnunia.

 

“Jambo jingine ambalo lilimkasirisha mwenye nyumba ni kumuona ‘Queen Darleen akimfanya mwanaye sherehe kubwa ya kutimiza siku arobaini tangu azaliwe huku akijua anadaiwa kodi,”chanzo chetu kilimwaga ubuyu.

 

Kiliongeza kuwa baada ya msanii huyo kuona mwenye nyumba kawa mbogo na hataki kitu kingine zaidi ya kodi na Queen Darleen hakuwa nayo keshi aliamua kufungasha virago na kwenda kuishi kwenye nyumba ya mama yake iliyopo Sinza.

 

“Kwa hiyo hadi sasa ‘Queen Darleen yupo nyumbani kwao Sinza na anapatikana muda wote hata ukienda utamkuta,” chanzo chetu kiliongeza.

 

Baada ya gazeti hili kupata tetesi hizo lilimvutia waya Queen Darleen ili kujua kwa nini ameamua ‘kurudisha mpira kwa kipa’ ambapo alijibu:

“Kama nimerudi nyumbani kuna tatizo gani, uzuri sijaenda kwa mtu, nimerudi kwetu.”

 

Hata hivyo, hakufafanua kurudi huko nyumbani kumetokana na madai ya kukosa fedha ya kulipa mwenye nyumba au kuna jambo jingine nyuma yake.

 

Aidha, kumekuwa na tetesi mitaani kwamba msanii huyo ambaye ni ndugu wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ siku za hivi karibuni ‘jua limewaka mfukoni’ kutokana na mambo ya kipato kuyumba. Mwandishi wetu alipokiuliza chanzo kuhusu ndoa ya msanii huyo alisema “ipo salama” lakini hali tu ndiyo ‘imechenji’.

Leave A Reply