The House of Favourite Newspapers

Dr Dre Asherehekea Talaka na Mkewe

0

HATIMAYE rapa maarufu na mtayarishaji wa muziki, Andre Romelle Young ‘Dr Dre’ (56) amefanikisha talaka ya kuachana na mkewe Nicole Young baada ya kudumu katika ndoa yao kwa miaka 25.

 

Dre na Nicole walioana mwaka 1996 na kufanikiwa kupata watoto wawili, wa kike Truly Young, 20, na wa kiume  Truice Young, 24.

Wawili hao wamekuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu na kuiomba mahakama kuvunja ndoa yao huku Nicole akidai kuwa amekuwa akinyanyaswa na mumewe huyo kwa kushushiwa kipigo na kutishiwa kuuawa mara kadhaa kwa kuwekewa bastola kichwani.

 

Aliongeza pia kuwa Dre alimfukuza Nicole ndani ya nyumba yao na kumfanyia vitendo vya udharirishaji wakati msanii huyo akiwa amelewa tungi lakini rapa huyo alikana kuwa hajawahi kumfanyia vitendo hivyo vya unyanyasaji.

Lakini ikumbukwe tu kwamba  amekua akituhumiwa mara kadhaa kutokana na kazi yake anayoifanya ya utayarishaji wa muziki.

 

Leave A Reply