The House of Favourite Newspapers

Ed Sheeran Akata Miaka Saba Bila Kutumia Simu

0

WAKATI mamilioni ya watu duniani kote katika karne hii wakitekwa na matumizi ya simu, hasa smartphones kiasi cha kushindwa kabisa kumaliza siku bila kushika simu, maisha haya tofauti sana kwa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Uingereza Edward Christopher Sheeran maarufu Ed Sheeran.

Ed Sheeran amefunguka na kusema kuwa, hajaigusa wala kuitumia simu yake ya mkononi kwa takribani miaka saba, yaani tangu mwaka 2015.

Ed Sheeran ameyasema hayo kupitia kwenye mahojiano yake na Collector’s Edition Podcast ka kueleza kwamba hatumii simu kwa kuwa ilikuwa kama sehemu ya kuharibu afya yake ya akili.

“Nilikuwa kama napata mzigo mzito hivi na huzuni nikiwa na simu yangu, natumia muda wangu kwa uchache sana, kitendo cha kuiacha simu nilikuwa ni kama nimekatia mahusiano na watu, kwa sasa natumia email pekee.

“Ni kwa siku chache sana nikipata muda natumia Laptop yangu kujibu email walau kumi pekee kwa muda huo kisha narudi kuishi maisha yangu.” alisema Ed Sheeran.

Wewe unaweza kukaa muda gani bila kushika simu yako?

Leave A Reply