The House of Favourite Newspapers

Enock Bella Afunguka Kusainiwa WCB / Nyumba Walizopewa Mmh! – VIDEO

Miongoni mwa Makundi ya Muziki yaliyowahi kutikisa Bongo ni Pamoja na Yamoto Band lililokuwa likiunda na vijana wanne, Aslay, Beka, Mbosso na Enock Bella, ambalo lilivunjika na kila mmoja kuanza kufanya kazi zake akiwa kama Solo Artist.

Global TV imemtafuta Enock Bella na kupiga nae stori kuhusiana na maisha yake ya muziki kwa sasa ambapo juzi tu ameachia kibao chake kipya kinachoitwa ‘I Swear’ na kinaendelea kufanya vizuri.

Enock amezungumzia uhusiano wake na wenzake watatu baada ya kundi kuvunjika na pia ameweka wazi kuwa anatamani kusainiwa lebo aliyosainiwa mwenzake Mbosso yaani WCB Iliyoko chini ya Mfalme wa Bongo Fleva Diamond Platnumz.

Comments are closed.