The House of Favourite Newspapers

Esma Amfanyia Petit Kitu Mbaya!

0

IRINGA: Esma Khan ni dada wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anadaiwa kumfanyia kitu mbaya aliyekuwa mumewe, Hamad Manungwi ‘Petit Man’.

 

Baada ya kutengana na Petit Man kisha kuolewa hivi karibuni, Esma anatuhumiwa kumuhamisha shule mtoto wao; Taraj bila kumpa taarifa mzazi mwenzake huyo.

 

Mbele ya Gazeti la IJUMAA, Petit Man amezungumza kwa uchungu kuwa, anakubaliana na kila kitu kilichotokea kati yake na Esma hadi kutengana, lakini kitendo cha kumuhamisha mtoto wao shule bila kumwambia yeye kama baba, siyo cha kiungwana hata kidogo, kwani yeye alikuwa akilipa ada ya mtoto wake.

 

“Kila mtu kuendelea na maisha yake, ni sawa kabisa, lakini kinachoniuma ni kumuona mwanangu Taraj mitandaoni akiwa amevalishwa sare za shule nyingine.

“Nimeamua kwenda shuleni alipokuwa anasoma, wananiambia amehamishwa, sasa kinachonishangaza mtoto ni wetu sote, lakini kama anataka nimuachie, pia aseme,” amesema Petit kwa uchungu mkubwa.

Petit Man anaendelea kusema kwamba, hakuna kitu kinachomuuma kama kunyimwa haki yake kwa mtoto wake, maana ugomvi ni wao kama wazazi haumuhusu mtoto.

 

“Nilishasema, hata tugombane kiasi gani, sipendi mtoto aingizwe maana yeye hajui lolote, lakini kama ameamua hivyo, sawa. Kama mtoto damu yangu, atanitafuta tu,” amesema Petit Man.

 

Petit na Esma walitengana miezi michache iliyopita kutokana na migogoro ya kila kukicha, ambapo Esma alifunga ndoa na mwanaume mwingine aitwaye Mswiza.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

 

Leave A Reply