The House of Favourite Newspapers

Esma: Familia Yetu Haina Tatizo

0

Baada ya kuwepo habari za hapa na pale kuhusiana na Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’, kurudisha majeshi kwa mama watoto wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, baada ya kusambaa habari kuwa Mondi anawasiliana na watoto wake, dada wa Mondi Esma Khan, amefunguka kuwa familia yao haina tatizo.

 

Esma amesema kuwa familia yao haina tatizo siku zote hasa linapokuja suala la watoto, maana watoto ndiyo wanakuza familia, hata linapokuja suala la wazazi kugombana na kupatana ni jambo la kheri, na mwanamke atakakuwa na kaka ake yeye anasapoti.

 

“Sisi familia yetu haina tatizo, hasa katika suala la damu yetu, hata wazazi wakigombana na kurudiana ni jambo zuri tu, japo mi si msemaji wa Diamond, ila kama dada yake nasapoti mwanamke atakaechagua kuwa nae, nasapoti furaha yake pia’’, alisema Esma.

Stori: Happyness Masunga

Leave A Reply