The House of Favourite Newspapers

Exclusive: Dakika 26 za Mama Anna Mghwira Nyumbani Kwake Baada ya Kuapishwa (VIDEO)

0

SAA chache baada ya Anna Mghwira kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Ikulu jijini Dar es Salaam, Global TV Online ilipata wasaa wa kufanya naye mahojiano maalum.

Mahojiano hayo exclusive, yalifanyika jana usiku, Ubungo-Makuburi mahali alipofikia baada ya kuapishwa na Dk. Magufuli, ambapo mapema asubuhi ya leo alitarajia kuondoka jijini Dar kwenda Mjini Moshi, yalipo Makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro, tayari kwa maandalizi ya kuanza kazi rasmi.

Katika mahojiano hayo, pamoja na mambo mengine, Mama Anna Mghwira aliieleza Global TV Online mazingira yote ya uteuzi wake na kwa namna ambavyo alipokea na pia kutoa ufafanuzi wa kina juu ya sababu za kukubali uteuzi wake na jinsi atakavyofanya kazi, katika kuhakikisha anasukuma gurudumu la maendeleo kwa Mkoa wa Kilimanjaro, kama ambavyo ilani na sera za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla, zinavyoelekeza, huku akiwataka wakazi wa mkoa huo kumpa ushirikiano wa kutosha.

Mama Anna Mghwira, ni mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, ambaye katika mbio za Uchaguzi Mkuu uliopita, aligombea na nafsi ya urais kupitia chama hicho, ambacho kiongozi wake mkuu ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Kitaaluma, Mama Anna Mghwira ni mbobezi wa masuala ya kijamii aliye pia mwanaharakati na msomi wa sheria za Haki za Binadamu, kabla ya uteuzi wa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alikuwa akifundisha vyuo mbalimbali kwa kujitolea pamoja na kuenedeleza harakati za maendeleo.

Leave A Reply