The House of Favourite Newspapers

Exclusive: Rapa T.I Ndani ya Albamu ya Harmonize (VIDEO)

Msanii wa Lebo ya WCB, Rajab Abdul Kahali maarufu kwa jina la Harmonize ama Konde Boy amefunguka juu ya baadhi ya mastaa wam Marekani na Afrika ambayo amewashirikisha kwenye Albamu yake mpya itakayoingia sokoni mwakani 2019, miongoni mwao akiwemo Clifford Joseph Harris Jr ‘T.I’ kutoka Atlanta nchini Marekani.

 

Harmonize amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika Kituo cha Radio cha Capital Fm nchini Kenya na kusema kwamba; “Albamu yangu itakwenda kubadilisha industry nzima ya muziki wa Afrika Mashariki kwa sababu nimezoea kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti.

“Albamu yangu itakuwa imemshirikisha msanii mkubwa kama T.I, kutoka Marekani, Burna Boy, Sauti Solo, Eddy Kenzo najitahidi kufanya na wasanii kutoka pande tofauti”.

 

Harmonize alifunguka ilikuwaje mpaka akakutana na T.I na kufanya mchongo wa kolabo; “Nlikuwa Atlanta na Meneja wa T.I,  ni kama kaka yangu, na tulikutana pale, tuliongea na mwisho tulikubaliana kolabo na T.I, na sio kwamba ni Meneja wa T.I pekee, bali hata Travis Scott na Ludacriss, la msingi tegemeeni mengi”.

 

Albamu ya Harmonize inategemewa kuingia sokoni Mwaka 2019, licha ya tahere, jina la Albamu na nyimbo zitakazopatikana kwenye Albamu hiyo zikiwa bado hazijaanikwa.

VIDEO: MSIKIE HARMONIZE AKIFUNGUKA

 

Comments are closed.