The House of Favourite Newspapers

Fahamu sababu kuu za kukumbwa na kiharusi

0

article-2446633-0F244E0B00000578-125_634x466Kuna aina nyingi za ugonjwa wa kiharusi ambazo zinasababisha mtu kukumbwa na maradhi haya.

Leo tutaeleza machache kwa mfano mtu anaweza kupatwa na kitu kinachoitwa kitaalam Subarachnoid Haemorrhage, ambapo mpasuko wa mshipa wa damu hufanyika karibu na eneo linalozunguka ubongo linaloitwa Subarachnoid na mtu kupata kiharusi.

Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini, hali inayoitwa kitaalam Atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa Thrombosis hiyo.

Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo.

Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza kuathirika na tatizo hili ni pamoja na Arteri za Common Carotid na Interior Carotid Arteries na Arteri za Vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa Circle of Willis lililo katika ubongo, hivyo mgonjwa kujikuta akikumbwa na kiharusi.

Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgonjwa wa Sickle Cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha kiharusi.

Kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa Endocarditis) huweza kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.

Upungufu wa usafirishaji damu mwilini Systemic Hypoperfusion – Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha Ischaemic Heart Diseases au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje au kupungua kwa damu mwilini, kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa.

Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.

Shinikizo la damu la muda mrefu lisilodhibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo na mgonjwa kukumbwa na kiharusi.

Dalili za kiharusi

Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo lililoathiriwa. Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa Cerebellum itaathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za wazi kama vile kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.

Iwapo sehemu ya ubongo wa kati Cerebral Cortex itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea, kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri, kuwa na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wa kufikiri na kuchanganyikiwa.

Leave A Reply