The House of Favourite Newspapers

Faida ya kunywa maziwa mtindi

1
pouring milk in a glass isolated against white background
pouring milk in a glass isolated against white background

Maziwa yaliyochachishwa  maarufu kama mtindi ni miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida mwilini.

Virutubisho hivyo ndani ya mtindi ni  Calcium, Phosphorus, Vitamin B2), madini ya chuma, Vitamin B12, Pantothenic acid au vitamin B5, Zinc, Potassium na Molybdenum.

Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, huongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali kwani huongeza mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.

Aidha, mtindi umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni Vaginal Infections. Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwa nayo wanawake hao kabla yalitoweka.

Utafiti uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani Journal Of Nutrition, umeonesha kuwa unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.

Mtindi pia umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini LDL- bad cholesterol na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini HDL – good cholesterol, hivyo mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta Fat mwilini hivyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.

Mtindi bora ni ule uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.

1 Comment
  1. Sadick Muhagi says

    Asante sana!

Leave A Reply