The House of Favourite Newspapers

FANYA MAMBO HAYA KUJIZUIA KUNYWA POMBE

 

MWINGEREZA Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilichouzika sana cha ‘Reasons to Stay Alive’ anasema yeye akinywa pombe humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.

 

“Hata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasiokula nyama halafu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo,” anasema Haig

 

Anasema ni bora kutoka kwa sababu kule utashawishika tu na njia nyingine ni kama:

1.Nenda kwenye migahawa na si baa.

 

 

2.Fanya mazoezi tumia ule muda unaokuwa wazi.

 

3.Weka wazi kwamba hutumii pombe.

 

4.Epuka makundi au marafiki wanywaji.

 

5.Tafuta starehe katika kinywaji mbadala.

 

6.Badili sehemu ulizokuwa unaenda kupumzika awali na wajulishe watu wako wa karibu.

 

Mbali na ukweli kwamba pombe ni sehemu kubwa ama kinywaji kinacho furahiwa katika jamii zetu, utamaduni unabadilika.

 

Takwimu za hivi karibuni kupitia utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha London unaonyesha theluthi ya vijana wadogo hawanyi pombe kabisa.

 

Japokuwa vijana wadogo ambao wanasumbuliwa na afya ya akili pia wana.tatizo la unywaji pombe kupita kiasi.

 

Jennifer Griffin, mtaalamu wa afya ya jamii lakini pia meneja wa taasisi ya huduma ya akili ‘Turn2me’ anasema watu wanatakiwa kujikita katika kufanya mazoezi kama njia mbadala, lakini pia kuyapa kipaumbele mahitaji binafsi ya msingi.

 

Pombe inahusishwa na wasiwasi lakini pia hali ya kukosa raha funaha na kuwa na woga. Lakini kujichanganya ndiyo namna vijana wadogo hufanya ili kujiunganisha na watu na kutengeneza marafiki. Wasipojichanganya kwa kuhofia kunywa pombe wanaweza wakaanza kujitenga kisha wakaanza kuteseka na upweke.

 

Uelewa juu ya athari za kiafya unazidi kukua. Kila mmoja akubali. Mtu anaposema hataki kunywa pombe usimlazimishe wala usimwuulize mara mbili.

 

Comments are closed.