The House of Favourite Newspapers

Fella: Bongo Hakuna Msanii wa Kulinganishwa na Diamond

0

MENEJA wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella amesisitiza kwamba mwanamuziki anayewakilisha ndiye kigogo wa muziki nchini Tanzania.

 

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, Fella ambaye pia ni mwanasiasa alisema kwa sasa hakuna mwanamuziki anayestahiki kulinganishwa na Diamond Platnumz kote Bongo.

 

Meneja huyo aliwasihi Watanzania waache kujaribu kumshindanisha Diamond na wanamuziki wengine wa Bongo huku akisema kiwango chake ni cha kimataifa.

 

“Diamond ashindanishwe na mtu ambaye anaweza kustahiki kushindanishwa naye. Hapa Bongo jamani watu waache kwanza. Huko mwanzo tulikuwa tunatafuta numba, lakini sasa hivi ashakuwa mwakilishi wa taifa letu. Lazima tuwe wapana kidogo kuzungumzia hili. Tusiseme kwamba anaweza kashindanishwa na mtu fulani, hamna!” Fella alisema.

 

Fella alidai hata mmiliki wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize hajatosha mboga kuwekwa katika nafasi moja na bosi wake wa zamani.

 

“Watu wakimshindanisha Harmonize na Naseeb wanafeli. Harmonize ametengenezwa na Naseeb. Harmonize ana nafasi yake na Diamond ana nafasi yake zaidi. Diamond kwa Harmonize anasimama kama baba. Ukimfananisha mtu na babake ni uongo,” alisema Fella.

Leave A Reply