The House of Favourite Newspapers

Fursa ya kuwa Mwandishi na Mtangazaji wa Kitaifa na Kimataifa yapatikana MSPS

0

Chuo cha Mlimani Schoool of Professional Studies (MSPS) cha jijini Dar es Salaam, kimetangaza fursa ya mafunzo ya Uandishi bora wa habari na Utangazaji itakayowawezesha wahitimu kufanya kazi katika vyombo maarufu vya kitaifa na kimataifa.

Hassan Ngoma, mkurugenzi wa MSPS aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa chuo chake kimebadilisha mfumo wa ufundishaji ili kiwe tofauti na vyuo vingine kwa kuzalisha wasomi wenye sifa za kuajirika.

“Kwa kipindi kirefu MSPS kimekuwa kikitoa mafunzo katika taaluma mbalimbali, lakini changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ni vipi tutakifanya chuo chetu kuwa tofauti na vyuo vingine?
“Maana ukipita kila sehemu utaona mabango na matangazo kuhusu vyuo vikuu, kibaya zaidi hata kozi zinafanana, tumejipanga kufanya vitu tofauti na wengine, kwanza tumefungua studio nzuri ya kisasa ya kujifunzia utangazaji.
“Mbali na chuo chetu kuwa na wakufunzi wenye uzoefu, katika program hii maalumu tutatumia pia watangazaji maarufu nchini ambao watakuja kuwafundisha kwa vitendo wanafunzi wetu, tutakuwa na waandishi wa habari mahiri ambao watawapa uzoefu wanafunzi wetu ili wakihitimu wawe wameiva katika kufanya kazi siyo kufundishwa tena makazini.

“MSPS imeweka uhusiano mzuri na wamiliki wa vyombo mbalimbali vya habari, taasisi za umma na binafsi nchini wataowapokea wahitimu wetu ili kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, tunatoa wito kwa mtu yeyote anayependa kuwa mwandishi wa habari afike chuoni kwetu au awasiliane nasi kwa namba za simu 0715-200900.

“Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu. Chuo kimesajiliwa na NACTE kwa namba REG/BMG/036. Tunafundisha kozi kwa ngazi ya cheti na Diploma na kwamba muhula wa masomo unatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.
“Kozi nyingine zitolewazo na MSPS ni pamoja na Business Administration, Banking and Finance, Human Resources Management, Procurement and Supply, Accountancy, Information Technology,” alisema Hassan.

Leave A Reply