The House of Favourite Newspapers

Gabo Amtolea Mtu Uvivu

0

BAADA ya tetesi nyingi kusambaa mitandaoni kuwa staa wa filamu za Kibongo, Salim Ahmed almaarufu Gabo amemtelekeza mtoto aliyewahi kuzaa na msanii mwenzake, Husna Sajenti hatimaye amemtolea mtu uvivu.

 

Gabo anasema kuwa, yeye siyo mtu wa kuongelea sana mambo yake mitandaoni ndiyo maana siku zote yupo kimya, lakini kuna baadhi ya mashabiki ambao hawajui wanachokifanya mitandaoni ndiyo anaowapa makavu yao.

 

“Mimi siyo mtu wa kuweka mambo yangu mitandaoni kwa sababu hata nikifanya hivyo haitanisaidia chochote,” anasema Gabo.

Hivi karibuni, Gabo alimposti mtoto wake wa kiume aliyezaa na mke wake wa ndoa kisha shabiki akakomenti kwa kuandika;

 

“Na yule ndugu yake kwa Husna Sajenti ndiyo umemsahau?”

Swali hilo limemuibua Gabo na kumjibu; “Ukimkumbuka wewe imetosha.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply