The House of Favourite Newspapers

Gigy atokwa povu kisa Nay kumwambia anajiuza

0

GIGY (2)MAYASA MARIWATA

MUUZA nyago mwenye vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amejikuta akitokwa povu baada ya kubanwa maswali kuhusu staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kumbwatukia kuwa anapiga dili za kujiuza ambazo ndiyo zinampa jeuri mjini.

Showbiz: Nambie Gigy aka Mamaa wa Supu?

Gigy: Ushaanza nawe! Ndiyo mimi wengine fotokopi.

Showbiz: Hivi hii ishu ya Nay kukwambia unajiuza unaizungumziaje?

Gigy: Nay! Nay ndiyo kijitu gani? Ni hivi hata kama najiuza, dau langu lipo juu yeye hana uwezo wa kuninunua isitoshe namuona kama muimba Taarab tu haniumizi kichwa huyo.

Showbiz: Duh! Kwa hiyo ni kweli unajiuza?

Gigy: Umalaya ni kitu cha kawaida kwa wanawake hapa mjini, wee unashangaa nini kila mtu anajua dau lake mwenyewe, sasa nawezaje kukataa dili la pesa nyingi.

Showbiz:Kwa hiyo unajiuza kwa shilingi ngapi na kwa nini ujiuze hujui kwamba msanii ni kioo cha jamii?

Gigy: Hivi wewe umekosa kazi za kufanya enh! Unaniuliza mambo ya Nay au kujiuza maana sikuelewielewi hivi!

Showbiz: Yote tu unaweza kunijibu!

Gigy: Huyo Nay peleka huko! Maisha yangu nafikiria pesa ndefu, yeye na elfu ishirini zake hukohuko. Maisha sasa yanasonga mfano kwa sasa nimefanya ukarabati nyumba yetu iliyopo Mbezi na vingine vingi tu, sasa huyo anayepoteza muda kusema najiuza akae chonjo sababu yangu yananiendea poa, upo?

Leave A Reply