The House of Favourite Newspapers

Gigy Money Aongoza Mapokezi ya Mpinzani wa Mwakinyo – Video

0

BONDIA kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshibangu Kayembe usiku wa kuamkia leo Agosti 12, 2020 amewasili nchini kwaajili ya pambano lake la ubingwa wa Dunia WBF akipigana na Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambalo litafanyika siku ya Ijumaa, Agosti 14, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Msanii Wa Bongo Fleva, Gigy Money akiongea jambo na bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshibangu Kayembe (katikati).

 

Mapokezi ya Kayembe yameongozwa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Gigy Money katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

Akimpokea Mcongo huyo huku akiweka uzalendo pembenei, Gigy Moneya amesema ni shabiki mkubwa wa Kayembe na anaipenda Congo DR huku akitamba na kusema kuwa lazima Kayembe amkalishe Mwakinyo.

Leave A Reply