The House of Favourite Newspapers

Gigy: Nilishatoa la Moyoni

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema sasa hana tena kinyongo moyoni mwake na msanii mwenzake Faustina Charles ‘Nandy’ kwa sababu alishatoa ya moyoni.

 

Akipiga stori na AMANI, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake alisema kwamba siku zote inapotokea mtu amemkera au kumfanyia vitu visivyo na staha, humaliza hasira zake kwa kumwambia ukweli kisha baada ya hapo maisha mengine yanaendelea.

 

“Nilishasema yale ambayo nilitakiwa kusema, hivyo mimi sina kinyongo tena na huyo mwanamke, maisha yanaenda, tufanye kazi tuache maneno maneno,” alisema Gigy.

Stori: Memorise Richard

 

Leave A Reply