The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 23: Maagizo ya Waziri MKUU kwa Balozi wa Tanzania Nchini Zambia – VIDEO

Waziri mkuu Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Balozi Hassan Simba Yahya, ambapo amemtaka kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amemtaka balozi Yahya kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia baina ya Tanzania na Zambia sambamba na kuhamasisha wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kuboresha uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Balozi Yahya amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Italia nchini, balozi Roberto Mengoni ambapo mbali na mambo mengine ametoa mwaliko kwa wawekezaji kutoka Italia kuja kuwekeza nchini akiahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini.

Naye, Balozi Mengoni ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Italia, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza uhusiano huo na kusema kuwa wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa.

Comments are closed.