The House of Favourite Newspapers

Video: Yusuf Manji Afikishwa Kortini Kisutu, Apewa Dhamana

DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara maarufu nchini na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusufu Manji amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la kutumia dawa za kulevya.

Yusuf Manji akifikishwa Mahakanami, Kisutu.

Manji amefikishwa mahakamani leo Februari 16, 2017 ikiwa ni siku ya nane tangu alipojisalimisha na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alipoitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ili kuhojiwa.

Akisoma shtaka hilo, wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi alisema kuwa, Manji anashtakiwa kwa kosa moja la kutumia madawa ya kulevya aina ya heroine ambapo mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeya alisema kuwa kutokana na kosa hilo, dhamana iko wazi kwa mshtakiwa endapo atakamilisha masharti.

Manji alikamilisha masharti chini ya wakili wake,  Alex Mngongoro na kufanikiwa kupata dhamana ya bondi ya shilingi milioni 1o aliyodhaminiwa na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Aidha kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo,Machi 16, 2017.

Umati mkubwa wa watu wanaodhaniwa kuwa ni mashahabiki wa Klabu ya Yanga, ndugu jamaa na marafiki walifurika katika viunga vya mahakama hiyo wakifuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.