The House of Favourite Newspapers

Mchezaji wa Yanga, Godfrey Bonny ‘Ndanje’ Afariki Dunia

Mchezaji wa Yanga, Godfrey Bonny 'Ndanje' Afariki Dunia
Mchezaji wa Yanga, Godfrey Bonny ‘Ndanje’ Afariki Dunia

Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny maarufu kama Ndanje amefariki dunia katika Hospitali ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo.
Godfrey Bonny 'Ndanje' akiwa na wachezaji wenzake
Godfrey Bonny ‘Ndanje’ (wa pili kulia) akiwa na wachezaji wenzake
“Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki. Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga,” alisema Nsajigwa.
Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Prisons ya Mbeya. Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambako alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa.
Mwenyezi Mungu Ampumzishe kwa Amani

Comments are closed.