The House of Favourite Newspapers

GWAJIMA Afunguka Kila Kitu, Asema ‘Mkono Sio wa Kwangu’ – Video

ASKOFU Josephat Gwajima amekana kuwa ile video ya utupu inayosambaa si yeye, ni teknolojia imetumika na watu ambao amedai kuwa anawajua na wana nia mbaya na yeye.

 

“Niliona hizo video jana asubuhi ila sikutaka kuongea maana nilitaka kufanya uchunguzi nimjue mtu wa nyuma yake, sasa nimekuja kumpiga. Hata kama tukio hili lingekuwa ni la kweli, aliyerusha nia yake si nzuri, anajua mimi nina mke na watoto wakubwa na nina makanisa zaidi ya mia nne. Lengo la mtu huyu haliwezi kuwa zuri ni zaidi ya kunichafua,  ni lengo la kishetani.

 

“Hata kama video ile ilikuwa ni ya kweli, kutokana na kuwa aina ya video ile haipaswi kuonwa na kila mtu, basi unajua moja kwa moja kuwa nia ya huyo mtu si nzuri. Sasa mimi simpigi mtu aliyeko mbele, nilikaa kimya nimjue kwanza aliyeko nyuma, ili nimpige yeye.

 

“Ukiangalia ule mkono ni wa baunsa, sio mkono wangu mimi. Hata kwa kutumia akili tu, ni nani arekodi video akiwa anajamiiana halafu aisambaze yeye? Picha ya kifua wazi iliyotumika na kusambazwa ni picha ya familia niliyopiga nikiwa na mke wangu na watoto wangu. Na sio vibaya kupiga picha kifua wazi ukiwa na familia. Na picha ile nilipiga zaidi ya miaka 10 iliyopita.

 

“Uchaguzi unakaribia mwaka 2020, sasa kuna watu wanahofu kwamba ninaweza kuwa na sauti nikawazidi hivyo wanajaribu kuniharibia. Niwaambie tu, ndiyo wananiongezea sauti, na wamethibitisha kuwa mimi ni mwanaume wa kweli. Matendo ya kipumbavu anayo-design mpumbavu, unamjibu kipumbavu.

 

“Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa. Waliosambaza walidhani nitaaibika, kumbe ndiyo imeonesha kuwa nina uwezo na ni mwanaume kamili. Safari hii itakuwa kali kuliko ile ya zamani na mtajua Mungu yupo. Ninaomba mjiulize hivi ni mwanaume gani anaweza kujirekodi halafu atume mwenyewe?  Isitoshe, ule mkono ni wa baunsa.

 

“Ile ni teknolojia imetumiwa ya kuunganisha picha na video. Haiwezekani mwili uwe wa mwingine na kichwa kiwe ni cha mtu mwingine. Mimi nilijua vita imeisha kabisa kwa sababu mnapomaliza ugomvi hakuna sababu ya mvutano kuendelea. Kila mtu anatakiwa kuweka silaha zake chini,” alisema Askofu Gwajima.

VIDEO: MSIKILIZE GWAJIMA

Comments are closed.