The House of Favourite Newspapers

Hadija Kopa Abariki Ndoa ya Diamond na Zuchu

0

MALKIA wa mipasho Bongo, Hadija Omary Kopa amesema haoni tatizo kwa msanii Diamond Platnumz kumuoa mtoto wake Zuchu kwa kuwa sio ndugu wa damu.

 

Kopa amesema hayo akihojiwa na Wasafi TV baada ya tetesi zikusambaa katika vyombo kwa habari kwa wawili hao wapo kwenye mahaba mazito wako mbioni kufunga ndoa.

 

“Mimi sijui chochote jambo linaanzaga nyumbani kwa mtoto wa kiume na ndio mposaji na muoaji unaniuliza mimi, mimi sijui chochote. Lakini vile vile hata kama litakuwepo yule mwanaume yule mwanamke kuna tatizo gani? Kwani wale baba mmoja Mama mmoja si kila mtu na Baba yake na Mama yake kuna tatizo gani,” alisema Khadija Kopa.

Leave A Reply