Halaand Awavuruga Messi na Ronaldo

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani Erling Braut Haaland amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 20 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiwa na umri wa miaka 20 lakini pia katika idadi ndogo ya michezo 14, baada ya kufunga mabao 2 dhidi ya Sevilla jana usiku.

 

 

Halaand alifunga bao lake la 19 na 20 kwenye michuano hiyo usiku wa Machi 9, 2021, kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora dhidi ya Sevilla, mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, bao la kwanza alifunga dakika ya 35 bao la pili dakika ya 54 kwa mkwaju wa penati, mchezo huo ulichezwa katika dimba la Signal Idunal Park nchini Ujerumani.

 

 

Ushindi huo unaifanya Dortmund kufuzu hatua ya robo fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-4, baada ya mchezo wa kwanza nchini Hispania Dortmund kushinda 3-1.

 

 

Mshambuliaji huyo kinda raia wa Norway, mwenye umri wa miaka 20 ndio kinara wa ufungaji wa mabao msimu huu akiwa na mabao 10 na ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi, kuanzia msimu uliopita wa 2019-20 mpaka msimu huu akiwa na jumla ya mabao 20 akifuatiwa na Robert Lewandowski mwenye mabao 19.

 

 

Na mabao 2 aliyofunga dhidi ya Sevilla jana usiku yanamfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 2 kwenye michezo 4 mfululizo ya ligi ya mabingwa. Lakini pia amekuwa mchezaji wa kwanza kufikia idadai ya mabao 20 katika idadi ndogo ya michezo 14, na ndio mchezaji wa kwanza kufikisha idadi ya mabao 20 akiwa bado hajafikisha miaka 21.Tecno


Toa comment