The House of Favourite Newspapers

Maskini Robinho Sasa ‘Kuozea’ Jela

0

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Brazil, Robinho de Souza, ameshindwa rufaa yake katika mahakama ya juu nchini Italia, hivyo atalazimika kukaa gerezani kwa miaka 9 kufuatia kukutwa na hatia katika kesi ya ubakaji iliyotolewa hukumu mwaka 2017.

 

 

Robinho alishtakiwa mwaka 2013 kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 23 raia wa Albania kwenye sherehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake katika klabu moja ya usiku huko Milan, akiwa na kundi la wahalifu wanaojihusisha na ubakaji.

 

 

Jaji wa mahakama hiyo ya rufaa ameshindwa kutegua hukumu hiyo na kumtaka Robinho na rafiki yake Ricardo Falco, kutumikia kifungo hicho japo kawapa siku 45 za kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi kupata haki yao.

 

 

Winga huyu aliyewahi kuishangaza dunia, kwa kuondoka ghafla katika klabu ya Real Madrid na kwenda kujiunga na Manchester City, maamuzi ambayo hayakutegemewa na wengi kutokana na utofauti wa timu hizo mbili kwa nyakati hizo.

 

 

Robinho wenye umri wa miaka 37 kwa sasa nyota wa zamani wa vilabu kadhaa ikiwemo Real Madrid, Manchester City, AC Milan na Santos, pia alicheza kwa mafanikio makubwa timu ya taifa ya Brazil ‘Selecao’ akiichezea michezo 100 na kuwafungia magoli 28, ameshiriki kombe la dunia mara mbili mwaka 2006 na 2010.

Leave A Reply