The House of Favourite Newspapers

Rolls-Royce Mpya ya Mondi Yatua Dar

0

Staa wa Muziki Barani Afrika na CEO wa #WasafiMedia, SIMBA @diamondplatnumz ameamua kuvuta Ndinga ya ndoto yake Rolls Royce Cullinan SUV ya mwaka 2021.

 

Gari hiyo yenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani 330000 (Tsh. Milioni 763.25 ) kabla ya Ushuru, imepokelewa leo kutoka Bandarini na staa huyo baada ya kuiagiza tangu mwezi uliopita.

 

Diamond alishawahi kuweka wazi muda mrefu kuwa gari ya ndoto zake ni @rollsroycecars , hivyo sasa anaweza kulala usingizi Mnono kwasababu ametimiza moja ya ndoto zake.

 

Hii inakua Gari ya 3 ya kifahari kwa @diamondplatnumz kununua ndani ya Kipindi cha Miezi Miwili baada ya Kuvuta Cadillac Escalades mbili Wiki kadhaa zilizopita!

Leave A Reply