The House of Favourite Newspapers

Mdee Ana Kesi ya Kujibu Kuhusu ‘Kumfunga Breki’ JPM

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee, anayedaiwa kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli.

 

Uamuzi huo umetolewa leo Mei 28, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya kutupilia mbali hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi.

 

Inadaiwa Julai 3, 2017 katika ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA zilizopo mtaa wa Ufipa Wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

 

Leave A Reply