The House of Favourite Newspapers

TBS Yataka Taarifa za Wazalishaji Wanyaya Zisizo na Ubora

0

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wananchi  na wafanyabiashara wote nchini kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini wazalishaji wa bidhaa za umeme hususani nyaya, zisizo na viwango ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa upimaji na ugezi  wa Bidhaa kutoka TBS  Johanes Maganga alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam kufuatia malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara  juu ya uwepo wa baadhi  ya viwanda hapa nchini vinavyozalisha nyaya hizo zisizo na ubora na hivyo kutishia usalama wa wananchi pamoja na mali zao.

 

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Maganga alisema milango ya TBS ipo wazi wakati wote hivyo ni muda muafaka kwa wananchi, wafanyabiashara kwenda na kutoa taarifa juu ya uwepo wa viwanda vinavyozalisha nyaya hizo ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao

“Tunawakaribisha muda wote na kutoka mahali popote waje hapa ofisini kwetu  kutupa taarifa ya watu hao ili tuweze  kujiridhisha na kisha tuchukue hatua kali dhidi yao kwa kuwa sheria ipo wazi kwa yeyote anayeikuka taratibu zilizowekwa kisheria na mamlaka  husika” alisema Maganga.

Kwa mujibu Mkurugenzi wa upimaji na ugezi  wa Bidhaa, TBS imekuwa na utaratibu wa kutoa leseni za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za umeme kwa kuweka utaratibu wa viwango vinavyotakiwa hivyo kama kuna kiwanda chochote kinazalisha chini ya ubora hilo litakuwa ni kosa ambalo mhusika anapaswa kuwajibishwa jambo alilotaka litolewe taarifa pale linapojitokeza.

Aidha Maganga alisema pamoja na malalamiko hayo kutolewa, TBS haitakaa kimya na badala yake itaendelea na utaratibu wake wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara viwandani na kwenye maduka ili kuona kama viwango stahiki vinafuatwa ikiwa ni utaratibu wa usimamizi wa sheria zilizopo.

Hivi karibuni  kulijitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara  wa vifaa mbalimbali vya umeme jijini Dar es Salaam  wakidai juu ya  uwepo wa biashara ya nyaya   zisizo na ubora zinazozalishwa na baadhi ya viwanda hapa nchini na kuiomba Serikali kupitia Shirika la viwango Tanzania (TBS) kufanya msako viwandani na madukani ili kuwabaini wahusika

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Kariakoo, baadhi ya wafanyabiashara hao pamoja na wanunuzi wa bidhaa hizo wamedai kumekuwepo na wimbi la uzalishaji wa bidhaa hizo hususani nyaya za umeme za majumbani ‘wiring’ zisizo na viwango  unaohitajika.

Wafanyabiashara hayo waliojitambulisha kwa majina ya Rashid Salum pamoja na Frank Mtonga waliopo eneo hilo, walisema kumekuwepo na bidhaa hizo katika baadhi ya maduka ya kariakoo na hivyo kusababisha maduka yanayouza bidhaa zenye viwango bora kukosa wateja kutokana na wananchi wengi kukimbia kwa kigezo cha bei na kuzifuata nyaya zisizo na ubora kutokana na unafuu wa bei bila kujua athari zake.

“Kuna maduka mengi hasa maeneo ya mitaa ya Narungombe na maeneo mengine yanye maduka yanayouza bidhaa hiyo, wanauza nyaya ambazo hata ukizitamaza kwa macho utabaini kuwa hazina ubora, kigezo kikubwa kinachofanya wananchi wazikimbile ni unafuu wa bei” alisema Salum

Kwa upande wake Mtonga alisema yeye kama mfanyabiashara aliwahi kupokea lawama kutoka kwa baadhi ya wateja wake, waliomtuhumu kuwauzia nyaya zisizo na ubora, suala alilodai kuwa hakulifahamu kwa kuwa hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya nyaya hizo na viwango vyake.

Akitolea mfano katika suala hilo, Mtonga alisema kwa nyaya zenye ubora wa viwango ambazo zinauzwa kwa wastani wa Sh 100,000, huuzwa kwa wastani wa hadi 70,000 kwa nyaya zisizokuwa na ubora wa viwango na hivyo kuathiri ushindani wa bei katika sokoo huku pia zikileta madhara kwa wananchi yakiwemo ya nyumba kuungua.

Leave A Reply