The House of Favourite Newspapers

Hamisa: Hapana, Hatujam Rudiana

0

HAMISA Mobeto ni mwanamitindo na msanii maarufu wa Bongo Fleva ambaye amefunguka ni kwa nini huwa hasherekei Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) kama watu wengine.

Hamisa anasema kuwa, kwa miaka mingi katika Siku ya Wapendanao ilikuwa ya huzuni kwake mara baada ya kufiwa na baba yake mzazi, Hassan Mobeto.

“Kwa miaka michache ambayo imepita nimekuwa nikisherehekea Valentine’s Day na Ex wangu (enzi hizo alikuwa mpenzi). Kwa wale wanaonijua wanafahamu kuwa nilimpoteza baba yangu Siku ya Valentine.

“Kwa hivyo sikuwaga na tabia ya kusherehekea Vday kabla yake (EX). Alinifanya nipende Valentine,” anasema Hamisa; mama wa watoto wawili.

Anasema kuwa, mwaka huu alikuwa na shaka kama angesherehekea Valentine’s Day kwa kuwa tayari wametengana na mpenziwe ambaye alikuwa anasherehekea naye. Hata hivyo, Hamisa alipatwa na mshangao baada ya mpenzi wake huyo wa zamani ambaye hajatambulishwa kumuonesha upendo kwa kumpa zawadi.

“Alisema eti anajua siku hii huwa ngumu kwangu kwa hivyo akanipatia zawadi. Hapana, hatujarudiana. Ni vile tu ukiwa mtu mzuri watu hukukumbuka,” anasema Hamisa.

Leave A Reply