The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Mama Dangote amkubali Zuchu

0

Bi Sandra au Mama Dangote; ni mama mzaa chema wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye anajulikana kwa misimamo yake thabiti juu ya wanawake anaokuwa nao mwanawe huyo kimapenzi.

Mama huyo ambaye amepachikwa jina la Last Say ameibua gumzo kama lote baada ya kuonesha kuguswa na video ya chumbani hadi kitandani ya Diamond na Zuchu ambaye kuna tetesi kwamba wanatoka.

Video hiyo inawaonesha wakicheza muziki ambapo baadhi ya watu walikuwa ‘wakim-tag’ ili kuona ‘riaksheni’ yake.

Mama Dangote amepsoti video na kuandika; “Diamond na Zuchu wanasema twende kidole, mama kidole…”

Kitendo hicho cha kuposti video hiyo ikiwaonesha wawili hao chumbani na kitandani kwa Diamond kimekuwa gumzo kwa sababu kumekuwa na maneno mengi kwamba Mama Dangote hamkubali Zuchu awe mkwe wake.
Wengi wanasema ameanza kulegeza kamba.
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply