The House of Favourite Newspapers

Hatimaye P-Square Waungana Tena

0

HEADLINE kubwa ya entartainment Barani Afrika kwa sasa ni ile inayowahusu Kundi la muziki la P-SQUARE kutoka nchini Nigeria ambalo lilikuwa likiundwa na ndugu wawili Peter Okoye na Paul Okoye limerudi tena upya.

 

Hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo, mapacha hao kukutana kwa mara nyingine baada ya kutengana tangu mwaka 2016 kutokana na ugomvi wa kifamilia licha ya kusuruhishwa mara kibao lakini wawili hao walikuwa wamegoma kabisa kupatana.

 

Tofauti hizo ziliisha tangu wiki iliyopita Peter alipoonekana akiwachukua watoto wa kaka yake Paul ambao wanaishi nchini Marekani na kuwapeleka shopping.

 

Baada ya mapacha hao kukutana, sasa wanarudi kama mwanzo ingawa bado haijaeleweka hata muziki wataanza kutoa pamoja au laah.

 

Katika video inayosambaa mitandaoni inamwonesha Peter akisalimiana na kaka yake mkubwa Jude ambaye ndio alikuwa meneja wao, na baadae kusalimiana na Paul kwa furaha kubwa.

Leave A Reply