The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Wema wa Buguruni Akutana na Wema Sepetu OG – Video

0

BAADA ya kujinadi kuwa yeye ni Wema wa Buguruni na kwamba ni shabiki mkubwa wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, hatimaye miss huyo amekubali kukutana naye uso kwa uso binti huyo anayeishi Buguruni jijini Dar.

Wema wa Buguruni ambaye jina lake halisi ni Rachel Said, aliripotiwa wiki iliyopita na gazeti dada na hili la RISASI MCHANGANYIKO baada ya kuangusha bonge la sherehe yake ya kuzaliwa.

Kwenye sherehe hiyo, kutokana na umaarufu wake wa kuwa ‘Wema wa Buguruni’, aliuza vijora 300 kwa watu mbalimbali waliokuwa wanataka kuhudhuria sherehe yake hiyo ya kuzaliwa ambayo ilifunga mtaa kwa watu kusasambua kama hawana akili nzuri.

Baada ya habari hiyo kutoka, meneja wa Wema, Neema Ndepanya alimpigia simu mwanahabari wetu na kuomba amkutanishe na kwani inaonekana kweli binti huyo ana mapenzi ya dhati na Wema.

Bila hiyana, Wema na Wema wa Buguruni walipanga kukutana maeneo ya Sinza juzi Alhamisi ambapo walikutana na kufanya hafla fupi ya kutambuana, kula, kunywa na kubadilishana namba za simu.

Mwisho wa siku Wema aliahidi kuwa naye karibu na kushirikiana naye kwenye shughuli zake za sanaa pale itakapowezekana.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply