The House of Favourite Newspapers

Shigongo Akomaa na Elimu Buchosa, Atua Sukuma na Bodaboda – Video

0

 

MBUNGE wa Buchosa, Mheshimiwa Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa wamelazimika kupanda pikipiki kutembelea shule mpya ya Sekondari Sukuma iliyojengwa kwa nguvu za wananchi baada ya msafara wao kushindwa kupita kutokana na gari iliyokuwa imepakia saruji kupeleka shuleni hapo kuharibika na kuziba njia.

 

Kijiji cha Sukuma kilichopo kata ya Bukokwa kilikuwa kikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa  shule ya sekondari, jambo ambalo lilikuwa linawalazimu wanafunzi wa kijiji hicho na vijiji jirani kutembela umbali mrefu zaidi ya kilometa 16 kwa siku kwenda kusoma katika Shule ya Sekondari Bukokwa na wengine kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 20 kwa siku kwenda Shule ya Sekondari ya Nyakaliro.

 

Kutokana na hali hiyo, wananchi wa Kijiji cha Sukuma na vijiji jirani waliungana na kujenga majengo manne yenye madarasa manane na ofisi za tatu za walimu, maabara na nyumba ya mwalimu ili kuwasaidia watoto wao waweze kusoma karibu na maeneo yao, jambo ambalo litahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii na kupunguza utoro  na kuacha shule, pia itaongeza ufaulu kwa wanafunzi wa maeneo hayo.

 

Baada ya kufika shuleni hapo, Mh. Shigongo amewapongeza wananchi hao kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuahidi kukamilisha madarasa hayo haraka ili wanafunzi waanze kusoma mapema iwezekanavyo.  Huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo na amewasisitiza wananchi wa Buchosa kujitolea kwa moyo mmoja katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

 

 

Leave A Reply