The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye…Fuata Maelekezo-14

0

ILIPOISHIA GAZETI LA RISASI JUMATANO:
“Sasa mimi nitakuwa mke mdogo au mpango huo wa kuwa na mke baada ya mama Rehema kuondoka haunao…wewe niambie tu, mimi nitapokea yote lakini naomba sana nijue mwisho wangu kwako ndani ya nyumba hii,” nilifunguka.
Sasa sikiliza majibu yake…

TAMBAA NAYO MWENYEWE…

“Hivi Jamila…” alianza kwa kuniita…
“Abee!”
“Unavyoona wewe ni nafasi gani itakufaa ndani ya nyumba yangu hii ambayo wewe unaijua?”
Nilikaa kimya kwa muda wa dakika kama mbili kabla sijamjibu. Nilikuwa najifikiria nimjibu nini! Nijipe nafasi gani..!
“Mke,” nilijibu kwa mkato nikasubiri majibu…
“Mke?”
“Ndiyo, nataka niwe mke wako.”
Baba Rehema alicheka sana. Alicheka mpaka akakaa kitandani hali ambayo mimi sikuipenda hata kidogo…
“Sasa jamani mbona unacheka hivyo, maana yake nini?” nilimuuliza baba Rehema. Yeye akaendelea kucheka tu. Nilimwacha mpaka alipomaliza, nikamuuliza tena…
“Sikia Jamila. Wewe huwezi kuwa mke wangu, utaendelea kuwa nyumba ndogo ya kuiba tu kama hivi. Mimi siwezi kuoa msichana mrembo na mdogo kama wewe.”
“Kwa nini?” nilimuuliza kwa sauti iliyoanza kukosa amani kwa majibu yake hayo.

“Utanisumbua tu Jamila na mimi sitaki kabisa usumbufu wowote unaohusiana na mwanamke.”
“Jamani, sitakusumbua. Mbona uliniuliza kama nina wanaume mitaani hapa nikakukatalia. Wewe jaribu kuchunguza mwenyewe. Mimi sina mwanaume na wala sina tamaa ya kuwa na wanaume.”
“Kweli Jamila?”
“Kweli jamani mpenzi wangu, we niamini mimi,” nilimwambia baba Rehema huku nikimlaza kitandani maana si aliamka na kukaa.

Baada ya kulala mimi nikaamka na kukaa, nikiwa namkunakuna kifuani, nakipapasapapasa kifua mpaka akabadilika sauti. Ikawa nzito, nikajua mambo yanakwenda sawasawa kama ninavyotaka mimi katika mtego wangu…
“Ja…mi…la,” aliniita kwa sauti ya kukatakata…
“Abee…”
“Uko poa?”
“Ndiyo mpenzi wangu, niko poa kabisa…wewe je?” nilimuuliza yeye je ili nijue anajisikije kwa lile zoezi nililokuwa namfanyia…
“Da! Jamilia unan’tesa jamani, mikono yako ina joto zuri sana. Unavyonipapasa hivyo mwenzio nahisi kama nipo Marekani ya Kusini,” baba Rehema aliniambia huku akitetemeka, ghafla akanishika mkono na kunivutia kwake, nikaangukia kitandani, palepale kitendo bila kuchelewa…!
***
Siku hiyo  nililala chumbani kwa baba Rehema mpaka kunakucha. Nilipotoka chumbani ili kwenda kuanza kufanya kazi, si nikakumbana na Rehema bwana! naye anatoka chumbani kwake…
“Haa! We dada Jamila ndiyo nini hivyo kuingia chumbani kwa baba ‘angu?”
“Shii, nyamaza Rehema,”  nilimchimba mkwara mzito na kuweka vidole vyangu vya kulia kwenye midomo, akanyamaza.
Alijiandaa kwenda kuoga ili aende shule. Nilimwandalia chai. Kwa Rehema licha ya mama yake kuondoka lakini haikuwa kitu kigeni kwake, kwani kama ni chai siku zote namwandalia mimi. Kila kitu namwandalia mimi.
Baba yake alipotoka, Rehema alimfuata sebuleni…
“Baba…”
“Unasemaje mwanangu?”
“Mwenzio dada leo nimemwona akitoka chumbani kwako,” alisema Rehema bila haya wala soni achilia mbali aibu…
“Hiyo ndiyo salamu Rehema?” baba yake alimjia juu…
“Shikamoo baba…lakini dada alikuja chumbani kwako leo asubuhi.”
“Haya, nitamkanya asije tena.”
“Sawa baba, mimi nakwenda shule.”
Baba Rehema alikwenda kuoga, akaingia kujiandaa kwa kwenda kazini siku hiyo.
Niliingia chumbani kama mama mwenye nyumba, nikamsaidia kumvalisha, nikamuweka sawa tai, mkanda wa suruali na mambo mengine yanayomhusu mke kumfanyia mkewe, nikamshika mabegani, nikambusu na kumwambia kwa sauti ya mahaba…
“Kazi njema mume wangu.”
Hakunijibu, akaning’ang’ania sana kwa kunikumbatia huku akiniambia…
“Sweet, siwezi kuondoka hivihivi tu…jioni mbali na wewe umenishikashika hapa unategemea nini?”
“Kwa hiyo mume wangu unatakaje?” nilimuuliza nikimwangalia kwa macho ya kulegea. Niliyalegeza kwa makusudi kabisa.
Mara, nikamwona mwenzangu anafungua tai, anavua shati, anafungua mkanda wa suruali, mara…
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.

Leave A Reply