The House of Favourite Newspapers

Idriss Arudisha Milioni 500 za Big Brother

0

MCHEKESHAJI @idrissultan ambaye pia ni mfanyabiashara hapa Bongo amedai kuwa amefanikiwa kizirejesha Dola laki 3 (zaidi ya sh. milioni 500) alizoshinda Big Brother Africa mwaka 2014 nchini Afrika Kusini.

 

Inaelezwa fedha hizo zilipotea baada ya kuwekeza kwenye miradi ambayo haikuweza kuzaa matunda kutokana na kukosa uangalizi mzuri, huku mwenyewe akidai watu wake wa karibu ndiyo waliomwangusha.

 

Idris amesema fedha hizo alifanikiwa kuzirejesha rasmi mwaka 2018 baada ya kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha miradi mbalimbali.

 

“Ile dola laki tatu, nimekuja kuipata tena 2018, hiyo ni miaka minne baadaye, siku hiyo naenda benki wananiambia umetimiza dola laki tatu yako, wakaanza kunipigia makofi, ndiyo maisha,” amesema @idrissultan.

 

Ameongeza kuwa alipoenda Big Brother hakuwa na mpango kupata fedha, bali kupata platform, halafu aitumie kufanya vitu vyake vikubwa sana na ndicho kitu anachofanya hadi sasa.

Leave A Reply