The House of Favourite Newspapers

Ijue Siku ya Mateso ya Yesu Kristo

0

NA SALUM MILONGO| GPL

IJUMAA KUU ni siku maalum ya mwaka ambayo waumini wa dini ya Kikristo ulimwenguni kote wanaadhimisha kifo cha ‘Yesu Kristo’, ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu Siku ya ijumaa miaka zaidi ya elfu Mbili iliyopita.

Ijumaa Kuu ni sehemu ya juma kuu lilioanza kwa adhimisho la  Yesu Kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (Yaani Masiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki yaani Jumapili ya Matawi.

Ijumaa Kuu pia ni sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake (Ijumaa), kulala kaburini (Jumamosi), na hatimaye kufufuka kwa utukufu (Jumapili), kwa ufupi: Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka.

 

Leave A Reply