The House of Favourite Newspapers

Jamaa Anaswa Akichepuka na Mke wa Mtu, Afungwa Kwenye Gunia

0

Kisanga cha aina yake kimezuka katika eneo moja mjini Embu nchini Kenya baada ya jamaa kufungwa kamba miguuni na kutiwa ndani ya gunia hadi alipe faini baada ya kufumaniwa akichepuka na mke wa rafiki yake.

 

Taarifa kutoka nchini humo zimearifu kwamba jamaa huyo alikuwa na tabia ya kumyemelea mke wa rafiki yake wakati mume huyo akiwa zamu ya usiku kazini.

 

Njemba huyo alifika kwa rafiki yake na kumkuta mkewe akiandaa chakula cha jioni. Kwa kuwa mrembo huyo hakuwa na watoto pale nyumbani, jamaa alichukua fursa hiyo kumrushia mistari ya mapenzi.

 

Wawili hao walikubaliana na kuzama katika boma la nyumba ambalo halijaisha pale pale nyumbani ili kutenda amri ya sita, lakini wakiendelea na mambo yao, ghafla mtu aliingia kwenye boma hilo.

 

Alikuwa ni mke wa dada yule, jamaa alipoingia ndani hakuamini macho yake, moyo wake ulimdunda kwa mshtuko akatokwa na jasho shingoni. Naye mwizi wa mke wa jamaa akaduwaa na huku akibaki mdomo wazi kwa kufumaniwa.

 

“Ala! Ni wewe unamnyemelea mke wangu! Usishtuke, tulia tu. Sina haraka,” mume wa mtu alisema huku akiufunga mlango. Jamaa kwa upande wake alianza kuomba msamaha ila dua zake ziliambulia patupu.

 

Mwenye nyumba alichukua gunia kubwa na kamba, alimfunga jamaa yule miguuni na kumtia kwenye gunia bila jamaa kulalamika. Mke wa jamaa naye alijikunyata kama kuku aliyenyeshewa huku akitetemeka kwa woga. Lofa alipigwa viboko kadhaa kama ngoma huku akipigiwa mayoni kwa kile alichokifanya.

 

“Kama unataka amani utafanya mambo mawili sasa hivi ili nikiachilie. Kwanza utalipa faini ya KSh 100,000 kwa kumnyemelea mke wangu. Pili utamchukua mke wangu awe mke wako na unirudishiea mahari niliyomlipia,” jamaa alisema.

 

“Nimegindua wewe sio mwanamke mwaminifu. Chukua kilicho chako na uende kabisa. Sikutaki tena,” jamaa alimwambia mkewe. Taarifa zinadai kwamba jamaa alipopatiwa masharti makali na mwenzake, aliomba nafasi ya kuwapigia jamaa wamchangie pesa ili alipe faini ya maradi aachiliwe huru.

 

Wakati jamaa alipokuwa akiwashawishi wenzake wamchangie mke wa jamaa alikuwa chumbani akikusanya virago vyake ajipange kuondoka.

Leave A Reply