The House of Favourite Newspapers

Muna Love atishia Kujicharanga Mwili mzima

0

 

MWIGIZAJI wa Bongo Movies na mfanyabiashara, Rose Nungu almaarufu Muna Love anasema kuwa, anaona baadhi ya watu wamezidi kumshambulia kuhusiana na kujifanyia upasuaji sehemu mbalimbali za mwili wake, lakini ametishia kuwa ni bora wakanyamaza kwa sababu anaweza kujicharanga mwili mzima.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA akiwa nchini Uturuki baada ya kufanyiwa upasuaji wa mdomo, Muna anasema kuwa, watu wamuache na maisha yake maana kila kitu anachofanya ni kwa ajili yake na siyo maisha ya mtu mwingine.

“Waniache, wasinichukize maana naweza kujifanyia upasuaji mwili mzima na wasiniambie kitu chochote, waniache kwani ndiyo furaha yangu, waniache,” amefoka Muna ambaye mbali na mdogo pia hivi karibuni alifanya upasuaji wa kujiwekea dimpozi mashavuni.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply