The House of Favourite Newspapers

Jay Z: Hakuna wa Kushindana na Mimi

0

Kupitia Twitter Space wakiwa live kwenye group la mazungumzo na mwanamuziki Alicia Keys wakati akisherehekea mafanikio ya albamu yake mpya “Keys” na marafiki kupitia mtandao huo.

Rapa Jay Z aliweka rekodi akijitapa kwa kusema “Hakuna wa kupambana na mimi, nawaambia hakuna mtu yoyote kwenye sayari hii anaweza pambana na mimi kwenye verzuz iwe masaa mawili ama zaidi hakuna” amesema.

Jay Z amekuwa msanii mwenye jina na heshima kubwa kwa kipindi kirefu ambaye wasanii wengi wamekuwa wakitamani kufanya pambano la kimuziki na rapa huyo.

Wiki moja iliyopita rapa Rick Ross aliweka rekodi akisema kuwa anaweza kushinda kwenye Verzuz dhidi ya Jay Z na kuwa walau huyo ndio msanii wa hadhi yake.

Pamoja na kutamba kuwa hayupo wa kushindana naye Jay Z Pia aliendelea kwa kupongeza wazo la Verzuz na jinsi jukwaa hilo linavyotoa nafasi kwa wasanii.

Verzuz ni program maalumu iliyoanzishwa na watayarishaji mahiri wa muziki kutoka nchini Marejani Swizz Beats pamoja na Timberland ambayo hurushwa live kupitia Verzuz Tv.

Hii ni Program iliyotambulishwa katika kipindi cha janga la Covid19 kama Virtul Dj and Rap battle, inayohodhi mashindano ya kuchana kwa wasanii wa Hip Hop, ufundi wa mixing kwa D’js pamoja na watayarishaji wa muziki.

Leave A Reply