The House of Favourite Newspapers

Je Unakubali? Cassper Nyovest Asema Hakuna Rapa Mkali Zaidi Yake Barani Africa

Nikisema niwaulize wadau wa muziki wa Hip Hop kuwa kati ya AKA na Casper Nyovest nani mkali zaidi, tutabishana sana na wala hatutayamaliza.

Cassper Nyovest kwa upande mwingine ana mtazamo wa tofauti kabisa, yeye anaamini kuwa ‘hakuna rappa mkali’ barani Africa zaidi yake!

Kwenye interview aliyofanya hivi karibuni nchini South Africa na kipindi cha Slikour On Life, Cassper alisema kuwa anaamini hakuna mkali zaidi yake kwenye game nzima ya Hip Hop…

Nenda Marekani uwaulize kuhusu Hip Hop ya Africa, watakutajia jina moja tu na hiyo ni kwasababu ya vitu nilivyovifanya hapa, kuperform na kujaza ukumbi wa The Dome, Orlando Stadium, na vitu vingine vikubwa kama hivyo…” – Alisema Cassper Nyovest.

Aliendelea kufunguka na kusema kuwa hafikiri wala hana mipango yoyote ya kuondoka Africa…

Nafanya hivi vyote kutoka huku. Mfumo wangu umebadilika. Ni bora kubadilisha game kutoka nyumbani. Mimi ni msanii kubwa wa Hip Hop kwa Africa so kwanini nisifanye ninachokifanya kwa ubora zaidi huku huku? Wananijua mimi kwa ukubwa wangu Africa” – Cassper Nyovest.

Je, unakubaliana na maneno ya Cassper Nyovest? Tubonge kwenye comments hapa chini.

SOURCE: MTV Base.

IMETAFSIRIWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.