The House of Favourite Newspapers

Jela Miaka 20 kwa Kukutwa na Pembe za Ndovu

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 20 jela Alais Layeni kwa kosa la kukutwa na pembe au meno ya tembo.

 

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu Agosti 10,2020, mbele ya Hakimu Mkazi,  Simon Kobelo,  baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

 

Wakili wa serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa wa Manyara, Mutalemwa Kishenyi, alieleza kuwa mshtakiwa huyo alikamatwa Desemba 17/2019 katika kijiji cha Njoro wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara akiwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya  shilingi milioni 69,000,00 pasipo kuwa na kibali cha mkurugezi wa wanyamapori.

 

Kishenyi amesema katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2020, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambapo mshtakiwa alijitetea na kuita shahidi mmoja.

Leave A Reply