The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi Lapatiwa Vifaa vya Kuongozea Usalama Barabarani na Coca-Cola Kwanza Ltd

0

Mkurugenzi wake wa Logistic Mr. Haji Ally (kulia) ilimkabidhi vifaa hivyo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinodoni, Notker Kilewa kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Coca-Cola Kwanza Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Idd Azzan. 

 

 

KAMPUNI ya Coca-Cola Kwanza Ltd imetoa majaketi ya kuakisi mwanga (riflekta) zaidi ya 200 fimbo zenye taa za kuongozea magari 70 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuliunga mkoni jeshi la polisi katika harakati zake za kupambana na ajali za barabarani haswa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

 

Kampuni hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi wake wa Logistic Mr. Haji Ally ilimkabidhi vifaa hivyo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinodoni, Notker Kilewa kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Coca-Cola Kwanza Jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza kwenye hafla hiyo Bwana Ally alisema;

 

“Ikiwa kama ahadi yetu tuliyowahi kutoa ya kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha usalama barabarani unadumishwa leo tumeamua kutimiza ahadi hiyo kwa kutoa vifaa hivi kwa ajili ya kuongozea vyombo vya moto barabarani.

“Tumetoa majaketi 200 ya kuakisi mwaka mwanga (riflekta) kwa ajili ya askari wawapo barabarani na fimbo 70 zenye taa za kuongozea magari na tunaahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha usalama barabarani unaimarishwa.

Naye Kamanda wa Usalama Barabara Wilaya ya Kinondoni, Notker Kilewa baada ya kupokea vifaa hivyo aliishukuru Coca-Cola Kwanza Ltd kwa uzalendo wao kwa kutoa vifaa hivyo kwa jeshi la polisi na kuwataka wengine kuiga mfano wa kizalendo kama huo.

 

“Vifaa hivi vitatusaidia katika majukumu yetu ya shughuli za usalama barabarani hivyo nitumie tena nafasi hii kuishukuru kampuni hii kwa moyo wa kizalendo waliouonesha katika kutuunga mkono,” alisema Kamanda huyo.

 

Mwenyekiti wa Kamati kamati ya Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni Idd Mohamed Azzan aliyekuwepo kwenye hafla hiyo aliongezea kwa kuisifu Coca-Cola Kwanza kwa msaada huo walioutoa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya ambacho kina changamoto nyingi haswa katika suala la usalama barabarani. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply