The House of Favourite Newspapers

Jide Ataka Uchebe Akamatwe, Apigwe!

0

STAA wa muziki nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, ametaka Ashrafu Sadiki aliyekuwa mume wa msanii mwenzie Shilole akamatwe na kupigwa kutokana na kitendo cha ukatili alivyomfanyia msanii huyo.

Jaydee  ametuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter baada ya kuona taarifa ya Shilole juu ya kupigwa na mwenzi wake huyo.

“Huyu Uchebe naye ashikwe apigwe vizuri tu anyooke. Shenzi sana,” ameandika Lady Jaydee leo Julai 8, 2020.

Mapema leo Shilole alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa amekuwa mvumilivu na anapingwa mara kwa mara na mume wake huyo wa zamani.

Leave A Reply