The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kujifunza wakati mwalimu hayupo

0

studentsKatika ulimwengu wa kujifunza, kuna mambo mengi yanayoweza kukufanya ufaulu katika mitihani yako ili kwenda hatua nyingine ya masomo. Mambo hayo yanajumuisha afya ya mwili na akili ya mwanafunzi, mazingira mazuri ya kujifunzia na kubwa ikiwa ni uwepo wa mwalimu ambaye ndiye haswa huwa msaidizi wa yale ambayo mwanafunzi anapaswa kujifunza.

Kitaalamu mwanafunzi hupewa asilimia 70 za kujifunza huku mwalimu akipewa asilimia 30 za kumuwezesha mwanafunzi huyo kuelewa jambo hiyo ikiwa na maana kuwa bila mwalimu mwanafunzi mwenyewe anaweza akajifunza na kufaulu kwa asilimia 70.

Katika mazingira ya elimu nchini, wanafunzi mara nyingi hujikuta wakiwakosa walimu darasani kutokana na hali halisi  ya mifumo ya utawala ambapo utakuta shule nyingi zina walimu wachache au waliopo wakishindwa kufundisha kutokana na sababu mbalimbali zinazoikwamisha taaluma yao isitumike ipasavyo.

Lakini wakati hayo yanaendelea wanafunzi huwa ndiyo waathirika wa kwanza wa hali hiyo jambo ambalo linapelekea uwezo wao wa kufaulu kushuka na hatimaye kufeli moja kwa moja masomo yao.

Katika hali kama hiyo mwanafunzi mwenyewe anapaswa kujiongeza mara mbili zaidi ya wanafunzi wanaosoma shule zenye mazingira mazuri ya kufundisha ambapo hapo mwanafunzi anapaswa kujifunza mambo mbalimbali na kutumia asilimia yake 70 ya kujifunza kwa ufanisi mkubwa hasa kwa kufanya yafuatayo:-

Kujua mitaala ya masomo yake

Japo kuwa walimu wanaweza kuwa ni tatizo lakini mwanafunzi anatakiwa aulizie mitaala ya masomo yake na kujua nini akisome na kipi akiache ili kutopoteza muda kwa vitu visivyomhusu. Katika mitaala hiyo ndipo mitiririko ya mada za somo husika kwa mwaka mzima wa masomo ya darasa huoneshwa huku ikielezwa wazi kuwa mwanafunzi anapaswa ajue nini ili ajibie mtihani.

Kutafuta vitabu, ‘material’ au ‘notsi’

Hatua ya pili itakayofuata hapa ni kwa mwanafunzi mwenyewe kutafuta vyanzo mbalimbali vya yale anayopaswa kujifunza ambapo hapa anatakiwa kuchukua vitabu vya masomo husika, notsi au material kutoka kwa wanafunzi wanaomzidi, wanafunzi wa nje, walimu wao au kupitia maktaba na mitandaoni.

Kujifunza kutoka kwa wanaojua

Katika hatua hii, mwanafunzi anapaswa kuwatafuta kwa hali na mali watu wanaojua masomo hayo iwe ni wanafunzi wenzake, walimu walio tayari au kupitia tuisheni mbalimbali ili mwisho wa siku aweze kuingia kwenye mtihani akiwa sawa na mwanafunzi aliyefundishwa vizuri.

Baada ya kutimiza hatua hizo mwanafunzi atajikuta ana uwezo mkubwa na kufaulu katika kiwango kizuri kiasi cha kuwashangaza wengi ambao walikuwa wakibeza uwezo wake na pengine hata kuwapita wanafunzi wa shule za viwango vya juu na mifano hiyo ipo.

Leave A Reply