Jinsi ya kupika Maboga ya Nazi

BOGANakukaribisha mpenzi msomaji wangu katika safu hii ya Mahanjumati ambapo kutokana na meseji zenu leo tutajifunza kupika maboga ya nazi. Chakula ambacho ni rahisi sana kupika.

MAHITAJI 

Boga    moja

Nazi moja

Sukari kiasi unachotaka

Hiliki nusu kijiko

IMG_0296KUANDAA NA KUPIKA

Kuna nazi kisha chuja tui vikombe viwili weka pembeni.

Menya maboga kiasi ukipendacho.

Yakate  vipande vidogovidogo.

Washa jiko kisha bandika maboga yaache mpaka yaive lakini humwagi maji na hakikisha hayavurugiki.

Maji yakishaanza kukauka weka sukari kiasi ukipendacho na hiliki.

Mimina tui la nazi na uliache lichemke na kuiva vizuri.

Likishachemkia vizuri na kubaki na supu kiasi epua na chakula chako (maboga) kitakuwa tayari kwa kula.


Loading...

Toa comment