The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kutibu choo kigumu!

0

Juisi ya Aloe vera
Kama unasumbuliwa na choo, yaani kila ukijisaidia unapata choo kigumu tumia juisi ya Aloe vera, kunywa nusu kikombe cha juisi hiyo asubuhi na muda mchache kabla ya kupanda kitandani usiku baada ya kula.
Ukisha kunywa juisi yako kunywa maji glasi moja kulainisha makali ya kinywaji.

Papai
Hili ni tunda ambalo ukila ipasavyo, linasaidia sana kuondoa tatizo la kupata choo kigumu, papai halina kiwango kama unaweza kula hata zima kwa siku litakusaidia.

Machungwa
Machungwa nayo yanatajwa kutibu tatizo hili, ukishamaliza kula, unajiandaa kwa ajili ya kulala usiku, kula chungwa moja hadi mawili, kula kwako tunda hili kutakusaidia kuamka ukiwa na hamu ya kwenda haja, watu wengi huenda haja asubuhi na kuianza siku vizuri.

Juisi ya limao na chumvi
Glasi moja ya juisi ya limao ukichanganya na chumvi kidogo, inasaidia moja kwa moja tatizo la kupata haja ngumu hata kama ulikuwa hupati, basi utapata kwa haraka sana.

Juisi ya tangawizi
Juisi ya tangawizi pia inatajwa kuwa ina uwezo wa kuyeyusha chakula kwa haraka sana na kukufanya kupata choo laini, kwa wewe mwenye tatizo hilo jitahidi kutumia juisi hii wakati wa mlo au ukimaliza.

Leave A Reply