The House of Favourite Newspapers

JPM Akanusha Kifo cha Dkt. Mpango “Anaendelea Vizuri”

0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amekanusha taarifa za uzushi zilizosambazwa mtandaoni kuwa Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango kuwa amefariki dunia na kuwataka Watanzania kuachana kuogopeshana na kutishana na wachukue tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona huku wakiomba Mwenyezi Mungu.

 

 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Februari 19,2021 wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

 

 

“Ulipoingia ugonjwa huu wa kubana mafua mwaka jana tuliushinda kwa sababu tulimtanguliza Mungu pamoja na juhudi zingine mbalimbali, unapoona kitu huwezi kukitatua wewe muombe Mungu, Mungu ndiye muweza.

 

“Imefikia mahali sasa tunatishana sana. Leo asubuhi nilitumiwa Meseji na Waziri wa Fedha Dk. Mpango ambaye amelazwa Dodoma na ninaomba niiosome hapa kwa faida ya wale waliokuwa wana Twitt kwamba amekufa.

 

 

“Tumefikia mahali sasa tunatishana sana, leo nilitumiwa meseji na Waziri wa Fedha Dkt. Mpango, ambaye amelazwa Dodoma, na ninaomba niusome hapa kwa faida ya wale ambao walikuwa wana-Tweet kwamba amekufa na amenitumia leo asubuhi.

 

 

“Ameniambia Mh Rais asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea hao wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana.

 

 

“Mhe. Rais Mungu akubariki na akupe Neema na ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili, naungana na wewe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu Balozi Kijazi, Waziri Mpango, ni huyo ambaye aliambiwa jana amekufa,” amesoma ujumbe huo Rais Magufuli.

 

Leave A Reply