The House of Favourite Newspapers

JPM Amwaga Sh. Bilioni 9 Mwanza Kupanua Uwanja wa Ndege – Video

0
Rais Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mwanza.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kupeleka bilioni tisa mkoani Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege.

Rais Magufuli ameagiza hayo leo Oktoba 30, 2017 akiwa jijini Mwanza katika uzinduzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha wilayani Ilemela ambapo ametaka fedha zaidi ya bilioni tisa zipelekwe Mwanza katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe uwanja wa kimataifa.

“Nimesikia kuwa mkandarasi anadai zaidi ya bilioni tisa, sasa Waziri naagiza mwambie huyo mkandarasi kuwa wiki hii atapata hizo fedha zote bilioni tisa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, nataka uwanja huu uwe uwanja wa kimataifa akamilishe uwanja huu kabla sijamaliza muda wangu, kwani asipokamilisha ndani ya muda huo hapo atalala lele, nataka wafanyabishara wa samaki wasiende nchi zingine kwa ajili ya kusafarisha samakai zao’ alisisitiza Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema serikali yake imekusudia kuunda meli kubwa itakayobeba watu 1,200, na tani za kutosha na magari katika ziwa Victoria.

Rais Magufuli yupo jijini Mwanza katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo ziara hiyo imelenga kuzindua Daraja la Furahisha ambalo tayari limeshazinduliwa na baadaye atazindua viwanda viwili.

VIDEO: RAIS MAGUFULI AKIHUTUBIA

Leave A Reply